Sunday, 2 August 2015

SOMO KUHUSU MADHABAHU



SOMO LA MADHABAHU (KUNA MAENEO MATANO).
1.    Namna ya kufahamu madhabahu,
2.    Mambo yanayotendeka kwenye madhabahu ya shetani,
3.    Makusudi Mungu kuwa na madhabahu,
4.    Ili tuweze kumuona Mungu katika maisha ni lazima tumjengee Mungu madhabahu,
5.    Namna ya kumjengea Mungu madhabahu.


1.    NAMNA YA KUFAHAMU MADHABAHU
•    Ni jambo la muhimu kwa muombezi  kufahamu mambo yanayo fanyika katika madhabahu.

•    Madhabahu ni nini?
Madhabahu ni mahali pa juu palipoinuka pa kutolea dhabihu(zamani),watu walijenga madhabahu wakachinja wanyama na kuwateketeza juu ya hiyo madhabahu.
•    Madhabahu ni mahali popote mtu anapokutana na Roho, inaweza kuwa roho ya Mungu au ya shetani.
•    Shetani ameiga mambo mengi ya Mungu, misingi ambayo Mungu anaitumia ndiyo hiyohiyo  shetani anaitumia.
•    Kutoka 20: 24 Madhabahu inayojengwa kwa ajili ya Mungu Mungu anakuja na kukubarikia, Madhabahu inayojengwa  kwa ajili ya shetani inatumika kwa ajili yake, Madhabahu inayojengwa na shetani  inaleta laana.
•    Madhabahu ya Mungu inaleta Baraka.
•    Mungu alipomuumba mwanadamu alimfundisha juu ya kufanya madhabahu (kujenga) wakati ule wa Kaini na Abeli  Mwanzo  4: 1-5
•    Mwanzo 8: 15-22 Nuhu alivyotoka kwenye safina jambo la kwanza alimjengea Mungu  madhabahu. Akamtolea Mungu dhabihu kwenye madhabahu hiyo aliyo ijenga,
•    MSTARI wa 21 Bwana  akasikia harufu iliyompendeza toka kwenye madhabahu.
•    Mwanzo 9: 8-17 Bwana anajibu kwa sababu ya madhabahu ya Nuhu aliyoijenga. Hata leo tunayo majibu ya kutokana na madhabahu aliyo ijenga Nuhu. Kuna wakati wa kupanda na kuna wakati wa kuvuna, wakati wa mvua na wakati wa kiangazi.
•    Na tunapouona upinde tunakumbuka agano la Mungu na wanadamu.
•    Penye madhabahu ni mahali pa maagano,
•    Kutoka 17: 15-16 Musa alijenga madhabahu baada ya vita vya Joshua.
•    Hesabu 23: 14 Balamu alijenga madhabahu saba kutaka mawasiliano na Roho ya Mungu ailaani Israel, Mungu akasema hawezi kuwalaani Israel.
•    Wakati  umefika wa  sisi kutamka  maneno na kumjengea Mungu madhabahu.
•    Kuna madhabahu zinazotawala katika nchi hii ambazo shetani amezijenga.
•    Siku zimefika kujua madhabahu zilizopo katika nchi yetu na kuziharibu,kuvunja kila makubaliano na maagano yaliyofanyika.
•    Yer.  1:10
•    Kama usipoinua madhabahu na kumwinua yesu katika mji shetani  ataendelea kukandamiza.
•    Simama katika mji wako na mtaa wako toa tangazo mwambie Mimi……………………najua wewe shetani  unatawala  katika mji huu nina
Kutangazia  kuanzia leo hii katika jina la Yesu Kristo shetani  na kila kitu chako uondoke.
•    Anza kwa kuomba msamaha kwa Mungu kwa kuzembea na kutoa nafasi kwa shetani kutawala mtaa huu.
•    Simama  kinyume na kila dhabihu iliyofanyika katika mtaa huu na kuikataa katika jina la
Yesu na kuiondoka nakuiharibu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti.
•    Luka 11: 1-4 Wanafunzi  wanamwambia  Yesu  utufundishe  kuomba. Hili ndilo andiko
Linalotufundisha kuomba.
•    Tunaposema Baba yetu,tunaweka uhusiano kati ya baba na motto. Tunapaswa kukumbuka Mungu ana ufalme duniani.
•    Zaburi 24: 1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.
•    Maombi  yanapaswa kutumika kuleta ufalme wa Mungu ulimwenguni lazima tuutafute ufalme wa Mungu ulimwenguni .
•    Warumi 12: 1-2 Kuitoa miili yetu kuwa dhabihu hata katika kufikiri kwetu na kubadilisha ili tujue mapenzi ya Mungu kwetu.
•    Ni lazima tuyatoe maisha yetu na kufanywa upya nia zetu. Sisi tutafute kujua mapenzi ya Mungu kwetu.
Tunapomtafuta ndipo Mungu anafunua mapenzi yake kwetu.
•    Na tunapojua hivyo hata maombi yetu hayatakuwa magumu sana kwetu.
•    Maombi ndiyo kodi ambayo  Mungu anayatumia kutumia bajeti yake.
•    Ufunuo 8: 1-5 Madhabahu inawakilisha kile kiti cha Enzi cha Mungu. Na kuona malaika wanaangalia na kupokea maombi, kile kilichomo ndani yake wanamimina katika dunia.
•    Hakuna  kitu kinachofanyika duniani ila ni maombi na uvumba toka kwa Mungu.
Ezekieli 22: 30 Mungu anamtafuta mtu duniani ampelekee maombi.
•    Ufunuo 5: 8-10 kuna wazee 24wanaokaa katika kiti cha Enzi na kuweka maombi ya watakatifu. Maombi ya watakatifu ni muhimu sana.
•    Ufunuo 1: 5-6 Yesu alikufa ili kutufanya sisi wafalme na Makuhani
Wafalme tumiliki katika nchi,
Makuhani  tumiliki katika madhabahu yake.
•    Mathayo 5: 8 Heri wenye moyo safi maana hao watamwona Mungu. Mungu anataka tuwe na moyo safi, Haki yetu izidi ile ya mafarisayo ili tuweze kumuona Mungu.
•    Makusudi ya moyo wako Mungu ayajue, usafi wa moyo wako ni muhimu sana
•    Galatia 5: 25 Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa roho.
•    Uthamani na jinsi unavyo ufikiria ufalme wa (Mbinguni) wa Mungu ni wa thamani sana kwako. Je! Ufalme wa Mungu una thamani gani kwako?


         2 .    MAMBO YANAYOTENDEKA KATIKA MADHABAHU YA SHETANI

•    Kumb 18: 10-12,
Kumb 13: 6-8
2 Falme 17: 17
•    Katika Madhabahu hizo watu wanakuja na kuwasiliana na roho ya shetani
Isaya 28: 15
Maombolezo 5: 7
•    Katika Madhabahu hizo kuna maagano yanafanyika na watu  wanaotoa kafara wanatoa watu, watoto, wanyama, mazao n.k.
Isaya 26: 21
Hesabu 35: 33
•    Shetani  amewadanganya babu zetu katika mila na desturi zetu katika kila madhabahu kunakuwa na  makuhani wanaohudumia mahali pale.
Kumb 13: 6-8
Kumb 18: 10-12
Walawi 20: 27
•    Kuhani husimama kati ya watu na Mungu, sisi ni makuhani wa kifalme.
•    Sisi kama watu tuliochaguliwa kama makuhani na tuyafanye yale ambayo tunatakiwa tuyatamke,
Isaya 8: 10
Yeremia 22: 29-30 unapoona mambo hayaendi sawasawa na Mpango wa Mungu hakuna haki inayotendeka, hata katika serikali n.k. Tamka neon maneno yako yana nguvu.
Isaya 49: 1-2
Mathayo 18: 18 Lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa


3.    MAKUSUDI YA MUNGU YA KUWA NA MADHABAHU

•    Zaburi 115; 16 -17
•    Mwanzo 1 : 26 – Dunia ilijengwa kwa sababu ya wanadamu ili waweze kumsifu Mungu
na kumwabudu.
•    Mwanzo 12: 1 -9 – Maisha ya Abrahamu yalikuwa ya kutembea kabla hajamiliki nchi aliyopewa. Abrahamu alitengeneza madhahabu ya kwanza madhahabu ya eneo
•    Madhahabu za kifamilia na za kikabila hizo madhahabu zina nguvu katika familia.Kuwa mwangalifu kwa mambo ya mila tunzojiingiza
•    Mwanzo 13:14-18 unapotembea katika mji na kutoa (Unabii) maneno ya kinabii, maneno haya yanakuwa na nguvu sana.
Mwanzo 15:8-9/ 18-21
Mungu anathibitisha tena juu ya ahadi yake, juu ya Ibrahimu.
•    Ibrahimu anamwambia Mungu nitajuaje kuwa utanipa lini hii nchi? Mungu anamwambia nijengee madhabahu.
•    Mwanzo 26: 23-25 Isaka pia alijenga madhabahu ya Mungu.
•    Mwanzo 28:11- 15, 21 Yakobo ni Mjukuu wa Ibrahimu wakati anamkimbia kaka yake Esau baada ya kumuibia uzaliwa wake wa kwanza.
•    Analala eneo ambalo babu yake Ibrhimu alimjengea Mungu madhabahu
Mstari 16 Yakobo akasema kweli Mungu yupo mahali hapa.
Mstari 12 Malaika walikuwa wanapanda juu na kushuka ina maana Malaika walikuwa hapo chini wakilinda.
•  Mwanzo 32: 1-2 Yakobo tena anakutana na malaika alipokuwa anarudi, eneo hilo ni maeneo ambayo babu yake ibrahimu alikuwa anamjengea Mungu madhabahu.
•    Unapomjengea Mungu madhabahu panakuwa ni malango ya mbinguni.
Mathayo 16: 18 nitalijenga kanisa langu na malango ya kuzimu hayatalishinda.
•    Ni muhimu sana kwa kanisa kujua malango ya kuzimu.
•    Kuna madhabahu inayovuta giza. Ni vigumu maeneo mengine watu (kuokoka) kupokea wokovu kwa sababu ya madhabahu zilizopo.
•    Watu wengine wanatumia madhabahu kuweka ulinzi katika maeneo wanayoishi.
Kutoa sadaka kabla hawajajenga nyumba
•    Sisi ni makuhani wa Bwana ni lazima tuchukue hatua kukataa nguvu za madhabahu nyingine.
•    Kumb 28: 43 Mgeni atakua na nguvu kuliko wewe mwenyeji leo hii tunaona wageni ndio wenye nguvu katika nchi yetu wanatutawala.
•    Mwanzo 33;18-20 Yakobo alinunua nchi. Mstari 20 akamjengea Mungu Madhabahu.
•    Unaponunua ardhi usivamie tu na kujenga vunja kwanza madhabahu ya Shetani na umjengee Mungu Madhabahu.
•    Mwanzo 35:11-14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema na Mungu, nguzo ya mawe akaimimina sadaka ya kinywaji na mafuta juu yake.
•    Maeneo mengi ya milima huwa shetani anayatumia kwa Madhabahu yake.
Zaburi 24:1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana Vilima na vyote ni mali ya Bwana.
•    Inawezekana Madhabahu nyingine ipo ndani ya mwili wako.
•    Mfano: kuchanja chale hizo ni Madhabahu za shetani inabidi kuzishughulikia.
Walawi 19:28
•    Juu ya kutofanikiwa katika maisha au familia yako.
Chukua hatua muulize Mungu.
•    Pia kuna Madhabahu ya kitaifa. Hii inafanya kazi sana, na hii hatuwezi kuishughulikia mpaka tuwe katika umoja.


4. ILI TUWEZE KUMWONA MUNGU KATIKA MAIMSHA YETU NI  LAZIMA TUMTENGEE MUNGU MADHABAHU

•    Mwanzo 28: 10-15 Yakobo alipokuwa anamkimbia ndugu yake Esau anakutana na
malango ya mbinguni mahali alipolala aliona ngazi na Malaika wanapanda na kushuka.
•    Madhabahu inafungua malango ya Mbinguni.
Unapomjengea Mungu Madhabahu katika maisha yako unafungua malango ya Mbinguni kwa kuweza wewe kuwasiliana na Mungu.
•    Shetani naye huiga vitu vya Mungu.
Unapokuwa na madhabahu ya shetani, na yenyewe ina malango yake na yeye kuweza kukutumia ipasavyo.
•    Babu zetu walikwenda kwa shetani kufanya agano naye.
Isaya 28:15 Tunafanya agano na mauti na kupatana na kuzimu.
•    Unapoenda kwenye Madhabahu ya shetani kuna karama zake: Ulevi, wizi, uasherati na uzinzi, uchawi, uongo, masengenyo n.k.
•    Shetani ameiga vitu vingi vya Mungu.
Mungu alimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake sadaka na shetani anawaambia watu watoe watoto sadaka.
•    Fanya utafiti katika maisha yako ni mambo gani magumu ambayo yameshika maisha yako.
•    Fanya utafiti katika maisha yako na familia yako walikuwa wanafanya mambo gani katika ukoo wenu.
•    Kuna mambo magumu katika ukoo wenu ambayo hayafunguki
•    Mfano: Kutokuolewa au kuoa, kutokufanikiwa, magonjwa n.k.
Kutoka 20: 1-6
2Falme 17:17
•    Ni muhimu kuingia katika toba na kufunga na kuomba. Muulize Mungu katika mambo yaliyo magumu.
•    Toba ndiyo mlango wa kutokea,
•    Anza na toba, Toba inafungua malango.


TOBA INA KAZI KUU ZIFUATAZO
•    Inatupa uhalali wa kuelewana na Mungu.
•    Inatupa uhalali wa kumshughulikia shetani ipasavyo.
•    Inamwondolea haki shetani na kutuweka sisi katika nafasi nzuri ya ushindi.
•    Inatuwezesha sisi kuweka na kuanzisha mawasiliano mazuri na Roho Mtakatifu.
•    Hutuingiza katika neema ya Mungu
•    Humpa Mungu kibali au nafasi kuanza kufanya kazi na sisi.
•    Toba ikikamilika inaleta utimilifu wa utii wako. Isaya 57:15

•    Baada ya kuomba Mungu anayajua yaliyotendeka kwenye mila zetu.
•    Chukua jambo moja moja na kiri mbele za Mungu katika uovu uliofanywa na babu zetu.
•    Walawi 26:40-42.
•    Ebrania 7:9-10 Tulishiriki yale ambayo Babu zetu walifanya
•    Damu ya Yesu ni malipo makamilifu yaliyofanyika
Ebrania 9:11-15
•    Nenda kwa Imani na kuipeleka Damu ya Yesu
•    Kitu ambacho kitakutoa hapo ni maombi.
Ebrania 12:22-24 Damu ya Yesu inanena hata leo.
Hesabu 35:33 Damu ya kulipwa kwa Damu.
•    Kanusha, simama katika mambo ambayo Yesu aliyafanya pale Msalabani Kol: 2:14.
•    Kila jambo ambalo lilikuwa linafanyika katika maisha yetu shetani alikuwa anaandika.
Aliandika katika anga, nyota, mwezi, jua na ardhi.
•    MWanzo 1:26 Mungu alimkusudia mwanadamu atawale bahari na vitu vyote pia.
•    Zaburi 19:1 Amka mapema asubuhi utangaze ukuu wa Mungu.
•    Kanusha na kataa makubaliano yaliyofanywa na mababu zetu
•    Yer:10-11 Mwambie wewe sio Mungu wewe ni pepo.
•    Usiwe na haraka kwenye Madhabahu ya Bwana. Hii ni vita kiroho penye Madhabahu ya Bwana.
•    Kama akishindwa kuchukua dhabihu kwenye Madhabahu ya Bwana, atakuja kwako kukuchafua wewe. Anajua huwezi tena kusimama kwenye Madhabahu.
•    Anataka uchafuke usitoe kitu chochote kichafu katika Madhabahu ya Bwana.
•    Kutoka 20:24 Madhabahu inayojengwa kwaajili ya Mungu, Mungu anakuja kukubarikia.
•    Mahali ambapo panafaa kujenga Madhabahu ni mahali ambapo Mungu mwenyewe amepachagua.
•    Mwanzo 22:1-14 Mahali ambapo Mungu amepachagua akutane na wewe ni mahali ambapo Mungu anapaangalia.
•    Unapofika mahali pa kuabudia hutakiwa kumshirikisha mtu mwingine (au mahali pa matengenezo).
•    Ibrahimu hakumshirikisha Sara alipokuwa anakwenda kumtoa Isaka Sadaka.
•    Kuna mambo mengine Mungu anasema na wewe binafsi si vizuri kumshirikisha mtu mwingine. Unapoenda kwenye Madhabahu ya Mungu Yehova kuabudu unakwenda wewe mwenyewe binafsi
•    Lazima uwe makini unapoenda kumshurikisha mtu shida zako, kila mtu ana Mungu wake.
Amosi 5:21:27 Mungu anachukia makutano yenu na nyimbo zenu.
•    Ndani yao walikuwa na miungu mingine, waliokuwa wakiiabudu.
•    Hata sadaka yao haiwezi kuleta matunda kama kuna Mungu mwingine ndani yake.
•    Mungu alimkatalia Daudi asimjengee nyumba kwasababu mikono yake ilimwaga damu. Ndani ya Hekalu kuna Madhabahu.
•    Isaya 61:1 Mwanadamu ndio hekalu la Mungu.
•    1Kor. 3:16-17 Na roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ndani ya mtu imo madhabahu ya Mungu.
•    Mwanadamu kabla hajaokoka ndani yake shetani alishapanda kitu ndani yake mwanadamu.
•    Kabla ya kuvunja hiyo Madhabahu mwanadamu hawezi kushinda dhambi, hasira, chuki n.k.
•    Watu wengi wamefungwa na uongo n.k
•    Katika hili huwezi kusonga mbele katika mambo ya Mungu
Isaya 52:2-6 Mungu anasema jikung’ute mavumbi kazi ya kujenga Madhabahu ni yako mwenyewe sio Mungu.
Amuzi 6:16-32 Gideoni anamjengea Mungu Madhabahu.
•    Mungu anamwambia aende kwanza akabomoe Madhabahu ambayo baba yake aliijenga
•    Ukitaka kumjengea Mungu Madhabahu ni lazima kwanza ubomoe Madhabahu ambayo ipo. Mstari 26 Ukamjengee Mungu Madhabahu kwa taratibu zake.
•    Mungu anataka umjengee yeye madhabahu mahali anapotaka yeye.
Amosi 10:10-16 Ili Mungu huyu adhihirike itakupasa uiondoe Miungu mingine.
2Falme 10:17-27
•    Mjengee Mungu madhabahu 1Falme 18:30-40 Elia amemjengea Mungu madhabahu.


UBARIKIWE SANA


23 comments:

  1. Amina Mtumushi wa Mungu, mafundisho haya yamekuwa msaada kwangu. Nilikuwa sijui pa kuanzia lkn sasa namshukuru Mungu kwa Neema yake kwako kuandika makala hii. Mungu akubariki Sana

    ReplyDelete
  2. Amen.Ubarikiwe Yesu akuinue na kukukuza Kiroho.

    ReplyDelete
  3. Ubarikiwe sana mtumishi wa BWANA. Maandiko haya binafsi nilikuwa na hitaji. Manake hatuwezi kuzikomboa familia zetu au nchi bila kwanza kuiangusha madhabahu ya shetani nasi kama wafalme na makuhani kunena neno la kifalme na kikuhani juu ya familia zetu na taifa kwa ujumla. MUNGU apewe sifa na utukufu.

    ReplyDelete
  4. Kwel Kabisa Kaka Bariki
    Mungu na Azidi Kuitumia Huduma hii
    ktk Kupata mambo mengi yatayozid kutujenga kiroho

    ReplyDelete
  5. Nimejifunza kitu kikubwa sana kupitia andiko hili. Ubarikiwe Sana Mtumishi

    ReplyDelete
  6. Barikiwa Mtumishi wa Mungu kwa ajili ya somo zuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen sana @Emmanuel Msangi .Ubarikiwe Yesu akuinue na kukukuza Kiroho.

      Delete
  7. Barikiwa Mtumishi wa Mungu kwa ajili ya somo zuri

    ReplyDelete
  8. Amen mtumishi wa mungu barikiwa sana

    ReplyDelete
  9. Yesu akubariki nimebarikiwa sana nimepata mwanga wa huduma yangu

    ReplyDelete